AHSANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, July 27, 2011

SHEREHE ZA MASHUJAA ZA HUDHURIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI MKOANI MTWARA:


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwaongoza viongozi wa Kiserikali wakati wa heshima maalum kwa ajili ya kuwaombea Mashujaa waliopigana vita katika aridhi ya nchi ya Msumbiji, ambapo jumla ya miili ya askari 101 walihamishwa kutoka Msumbiji mwaka 2004 na kuzikwa katika Makaburi Naliendele mkoani Mtwara kati ya 108 waliofariki katika vita hivyo. Sherehe hizo za kuwakumbuka mashujaa hao zimefanyika leo Julai 25, 2011 katika viwanja vya makaburi hayo mkoani Mtwara.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akikabidhiwa Mkuki ili auweke, katika Mnara wa Mashujaa mahala walipozikwa Mashujaa 101 waliopigana vita Msumbiji, ikiwa ni siku ya sherehe ya kuwakumbuka Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja hivyo vilivyopo Naliendele mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011.



Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya sherehe hizo.

0 comments:

Post a Comment