Jahazi lililokuwa linakadiliwa kuwa lilibeba watu wasiopungua ishirini na tano(25) lilizama katika fukwe za Mtwara katika bahari ya Hindi. Jahazi hilo lilikuwa linatokea mtwara mjini kuelekea Msanga Mkuu ng'ambo ya pili ya Bahari. Kati ya hao inakadiliwa watu zaidi ya kumi wamepoteza maisha, watano ni majeruhi wakiwemo walimu wawili, na kumi bado hawajaonekana. Maelezeo ya awali ya wahanga wa ajali hiyo wanadai imesababishwa na mzingo mkubwa uliokuwa umebebwa katika jahazi hilo. Kwa maoni ya wananchi wa eneo hilo wanasema serikali yao ya awamu ya nne iliwaahidi kuwapatia kivuko cha uhakika kinachotumia mashine. Wananchi hao wameongea na mtwara leo na kusema zinahitajika juhudi za haraka iwezekanavyo kuwahisha kivuko hicho kabla maafa zaidi hayajaendelea kutokea kwani mahitaji ya watu wa eneo la Msanga Mkuu yameongezeka na hivyo sehemu kubwa ya shughuli zao hufanyika Mtwara mjini.
0 comments:
Post a Comment