AHSANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, July 27, 2011

SHEREHE ZA MASHUJAA ZA HUDHURIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI MKOANI MTWARA:


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwaongoza viongozi wa Kiserikali wakati wa heshima maalum kwa ajili ya kuwaombea Mashujaa waliopigana vita katika aridhi ya nchi ya Msumbiji, ambapo jumla ya miili ya askari 101 walihamishwa kutoka Msumbiji mwaka 2004 na kuzikwa katika Makaburi Naliendele mkoani Mtwara kati ya 108 waliofariki katika vita hivyo. Sherehe hizo za kuwakumbuka mashujaa hao zimefanyika leo Julai 25, 2011 katika viwanja vya makaburi hayo mkoani Mtwara.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akikabidhiwa Mkuki ili auweke, katika Mnara wa Mashujaa mahala walipozikwa Mashujaa 101 waliopigana vita Msumbiji, ikiwa ni siku ya sherehe ya kuwakumbuka Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja hivyo vilivyopo Naliendele mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011.



Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya sherehe hizo.

Sunday, June 19, 2011

Karibu Mchangani Internet Cafe Mtwara


The best Internet Cafe in Mtwara

Sunday, November 21, 2010

MAMBO MSWANO KILA KI2 KIPO POUWAZ



Wadau musione kimya, kaeni mkao wa kula kwa mambo makubwa ya Mtwara leo ni mpango mzima

Thursday, August 5, 2010

MMH..KWELI TUNADUMISHA UTAMADUNI HAPA....??


Hakika kudumisha utamaduni wa Mtanzania kwa njia hii sina comment , au wadau munasemaje.....?

Tuesday, August 3, 2010

O'SHEA AKIWA NA WAKALI NDANI STUDIO YA PC FM


Me nikiwa na Mkali wakusini upande wa kulia Muite Pasha,akifuatiwa na Qj,anaefuata ni m2mzima O'shea pembeni yangu Makamua ndani ya studio ya Pc, hawa jamaa Makamua na mwenzake Qj hawa ndio wanaounda kundi la Wakali kwanza ambao hapo mwanzo walikuwa na Joslin lakini kwasasa wanasemaJoslin hayupo tena kundini kutokana na kuamua kujiondoa katika kundi hilo la wakali kwanza.

HAWA NI BAADHI YA WANAONIPA SAPOTI YA KUTOSHA KWENYE MEDIA


T plus akiwa Joel Shija (Mtoto wa dada Mayi )kama apendavyo kujiita wanaipa shavu la kutosha Blog yetu ya Mtwaraleo ili iweze kufahamika katika kituo cha redio cha Pc FM kilichopo hapa Mjini Mtwara , bila kumsahau Dj Askofu ambaye naye alinisaidia sana ahsante sana kwa msaada wako bro.

BARA BARA YA MTWARA - DSM


Hali ya bara bara yetu ya Mtwara mpaka dsm inaenda kwa kasi kubwa sana baada ya mkandalasi kutishiwa kupigwa stop baada ya kuchelewesha kumaliza kazi, kwa hakika hali halisi tunaiona hasa huku kusini(mkoa)mambo haya kuwa shwari enzi hizo ukilinganisha n hali yaaa hivi sasa inaonyesha dhali Serikari yetu ilivyo simama kidete, ilikuwa unachukua hata wiki moja kusafiri kutoka Mtwara kwenda Dsm kutoka na njia mbovu, kwa sasa tunashukuru mungu kuona unachukua masaa kusafiri.


kama kawaida barabara inavyoenda kwa kasi


Dah.... kwa hakika juhudi zinaonekana kuwa kweli Serikali haitaki muchezo


Unabishaaaaaaaaaa kweli tunajipangusa kuhusu barabara yetu, big up... au munasemaje wadau?

Thursday, June 10, 2010

LEO WADAU TUJIKUMBUSHE KIDOGO HISTORIA YA KAMJI KETU

Mtwara ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mtwara. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 92,602 .

Mtwara ni mji wa bandari kando la Bahari Hindi karibu na mpaka wa Tanzania na Msumbiji. Kiutawala Mtwara ni wilaya ya Mtwara mjini umeunganishwa pamoja na mji wa kihistoria wa Mikindani katika halmashauri ya manisipaa ya Mtwara-Mikindani.

Historia

Mtwara ni mji mpya ulioanzishwa tangu 1947 mahali ambako palikuwa na kijiji kidogo cha wavuwi tu. Waingereza waliotawala Tanganyika wakati ule walipanga mradi mkubwa wa kilimo katika Tanganyika ya Kusini wakahitaji bandari kwa ajili ya kubeba mazao yake. Mji ulipangwa kitaalamu kwa ajili ya wakazi 200,000 na mahali palichaguliwa kwa sababu ya badari asilia iliyofaa hata kwa meli kubwa.

Bandari ilijengwa na mji mpya ulianzsihwa lakini tangu 1950 ilionekana ya kwamba mradi wa kilimo kilishindikana. 1953 mji ulikuwa na wakazi 36,999 pekee. Mji haukuendelea ukarudi nyuma hasa kwa sababu pwani la Kusini ilikosa barabara na njia za mawasiliano. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Msumbiji ilizuia biashara ya mpakani.

Tangu miaka ya 1990 uchumi ulianza kusogea mbele polepole. Barabara ya lami inaendelea kutengenezwa kutoka Daressalaam kuelekea Mtwara. Tangu kukamilishwa kwa daraja la mto Rufiji mawasiliano kwa barabara yameboreshwa hata wakati wa mvua. Vilevile feri inayovuka mto Ruvuma imeongeza biashara ya mpakani na Msumbiji.

Kuna pia mipango ya kujenga barabara imara kutoka Mtwara kwenda Songea na Ziwa Nyasa itakayowezesha badari kuhudumia kusini yote ya Tanzania pamoja na Malawi.

Friday, May 28, 2010

SIDO KUKABIDHI VYETI WAHITIMU 22 MJINI MTWARA


Mbunge wa viti maalumu mkoani Mtwara, Anasitazia Wambura (kulia) akikagua bidhaa zilizosindikwa na kikundi cha wajasiliamali cha Kundecha cha mjini Mtwara, muda mfupi baada ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu 22 wa mafunzo ya usindikaji yaliyoendeshwa na SIDO. kulia ni Meneja wa SIDO Mtwara. Novertus Lihepanyam. katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Boma mjini hapa jana.

ZAIN KUTOA MSAADA WA VITABU KATIKA SHULE ZA MTWARA NA LINDI


Afisa elimu mkoa wa Mtwara, Epsoin Kipenya, alipokea vitabu kwa niaba ya serikali kuitoka kwa meneja wa Zain kanda ya Lindi na Mtwara.Bartholomew Masatu, Zain imetoa vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni nne kwa shule mbili za Mtwara na mbili Lindi kupitia mpango wake wa ‘building our nation’.


Afisa elimu mkoa wa Mtwara akimkabidhi vitabu Mkuu wa shule ya sekondari wasichana Mtwara, Marry Kaguo. muda mfupi baada ya kuvipokea kutoka Zain.

Thursday, May 13, 2010

SHEREHE ZA UFUNGUZI WA DARAJA LA UMOJA WA MSUMBIJI NA TANZANIA(MTAMBASWALA)


Huu ndiyo uhalisia wa umati wa watu waliohudhulia ktk uzinduzi wa sherehe hizi za ufunguzi wa daraja.


Huo ndiyo muonekano halisi wa daraja la Umoja jinsi gani linavyovutia na limegarimu Billion 34 mpaka kukamilika daraja hili


Bendi ya T.O.T walikuwa wakikonga nyoyo za wanainchi kuhakikisha mambo yanakuwa mswano.


Mh kwa hakika watu walijaa siyo kipole pole m2wangu.


Mh Rais wa Tanzania akiwa na Rais wa Msumbiji Mh Almando Gedbouza wakati braziband wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania


Hapa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili na msafara wa baadhi ya viongozi wa Tanzania Rais Mstaafu Mh Ally HAssani Mwinyi na Mh Benjamini William Mkapa pamoja na waziri wa miundo mbinu Mh Shukuru Kawambwa.

Wednesday, May 5, 2010

WAKALI KATIKA POUZ


Mr Blue akiwa katika pouz na mkali Cyril. Hapa ni maeneo ya Msemo katika Hoteli ya kitalii Mtwara, hapa ni baada ya Blue kukamua katika show iliyofanyika katika ukumbi wa Blantyre Mtwara, Ndipo alipokutana na Cyril na kuchill maeneo haya. Hongera sana kwa show ya Blue aliyekamua na Abby Skillz.


Hapa ni katika moja ya pouz za maeneo ya ufukweni dah! inapendeza sana. Karibuni Mtwara wadau muone maeneo ya kuvutia ambayo ukiwa huku utajisikia uko nyumbani huu ndio Mpango mzima unangoja nini? Tembelea Mtwara sasa utapata kile unachostahili kupata. Big up tena kwa blue na crew yake nzima kwani tunaamini watasaidia kuutangaza mkoa wa Mtwara have a gud time man.

Sunday, May 2, 2010

JAHAZI LAUA !!!!!!!!


Jahazi lililokuwa linakadiliwa kuwa lilibeba watu wasiopungua ishirini na tano(25) lilizama katika fukwe za Mtwara katika bahari ya Hindi. Jahazi hilo lilikuwa linatokea mtwara mjini kuelekea Msanga Mkuu ng'ambo ya pili ya Bahari. Kati ya hao inakadiliwa watu zaidi ya kumi wamepoteza maisha, watano ni majeruhi wakiwemo walimu wawili, na kumi bado hawajaonekana. Maelezeo ya awali ya wahanga wa ajali hiyo wanadai imesababishwa na mzingo mkubwa uliokuwa umebebwa katika jahazi hilo. Kwa maoni ya wananchi wa eneo hilo wanasema serikali yao ya awamu ya nne iliwaahidi kuwapatia kivuko cha uhakika kinachotumia mashine. Wananchi hao wameongea na mtwara leo na kusema zinahitajika juhudi za haraka iwezekanavyo kuwahisha kivuko hicho kabla maafa zaidi hayajaendelea kutokea kwani mahitaji ya watu wa eneo la Msanga Mkuu yameongezeka na hivyo sehemu kubwa ya shughuli zao hufanyika Mtwara mjini.

Thursday, April 29, 2010

UZINDUZI WA MSIJUTE SEA BREEZE RESORT


Kwa hakika hapa mwake pametulia , m2mzima nitakuwa ninatia timu daily pande hizi....


Unabishaa...mwanzo mwisho ndiyo hapo watu walijiachia full furaha pande za msijute


Dah... nikakutana na wadau wa Exim Benk wakiwa wanapata shavu lakutosha kama kawa


Mpango mzima ulikuwa hapa maana dah.....siwezi sema, mwenyewe wajionea


Dah.. jamaa walinipa saport ya kutosha kuhakikisha Mtwara leo inachukua snape ukizingatia wengi wao walikuwa hawataki nichukue snape thx kwa saport wakubwaaa....

Wednesday, April 21, 2010

BARABARA YETU DAR - MTWARA


Dah... kwa hakika jamaa wanaendelea vizuri na ujenzi wa barabara na kuhakikisha hii kero inamalizika kabisa kuhusiana na swala zima la usafiri ila kinacho waangusha ni mvua ambazo zinanyesha na ufanya hali ya barabara kuwa mbaya kwa sasa , kikubwa tuendelee kuomba mungu mpango mzima ukamilike au wadau munasemaje kuhusiana na hili swala......

Monday, April 19, 2010

DARAJA LA UMOJA WA MSUMBIJI NA TANZANIA(MTAMBASWALA)


Dah....hapa ukiaga kwamba unaenda kazini kweli unaenda kazini maana ni balaaaaa.


Mmh wanaume mzigoni dah.. kwa hakika kazi ilifanyika kweli.


Jinsi gani watu wakivyofanya kazi kuhakikisha mambo yanakaa vizuri juu ya swala hili


Daraja linavyoonekana kutokea Nchi ya Msumbiji kweli Umoja unapendeza.


Jinsi lionekanavyo kwa chini hiii ndiyo hali halisi ya hili daraja la umoja.


Kwa jinsi lionekanavyo kwa ukaribu zaidi jinsi lilivyo pendeza ...


Mwanzo wa daraja letu la Umoja upande wa Tanzania teh teh hapa mambo mswano ki2 mwake..

Friday, April 16, 2010

WAKUU NA WAMILIKI WA VETA KANDA YA KUSINI


Nisiku ya kongamano la kukutana wakuu wote na wamiliki wa vyuo vya VETA kanda ya kusini iliyofanyika hivi karibuni hapa Mjini Mtwara ktk chuo hiko vha VETA

UFUGAJI WA SAMAKI MTWARA VIJIJINI


Mzee akivua samaki ktk bwawa la samaki Tangazo Mtwara vijijini


Kikundi cha ufugaji samaki cha Tangazo Mtwara vijijini wakivua samaki ktk mabwawa hivi karibuni

TUTHAMINI TAMADUNI ZETU


Mcheza ngoma za Utamaduni akifanya makeke yake kwenye Tamasha hilo la MAKUYA


Wacheza ngoma wa kikundi cha Nyundo Mtwara vijijini, wakiwa wanacheza ngoma kwa ufasaha zaidi


Watalii wakichukua snape na kushangaa wasanii wanavyo cheza ngoma za utamaduni ktk tamasha la MAKUYA

Wednesday, March 31, 2010

MH....MAN UTD WENZANGU TUTAFIKA....????


Wadau kuhusiana na gemu ya jana munaionaje nafasi ipo ya kuchukua kombe au .....?
naomba maoni yenu wadau wenzangu

Tuesday, March 30, 2010

PANDE ZA MSEMO


Dah... wadau munasemaje khs mpango mzima wa msemo ....???


Pande hizi huanga ninatimba siku za week kubadilishana mawazo na wadau jamani khs swalazima la blog yetu ya Mtwaraleo

KWA SASA TUNA SHUKURU MUNGU KWA KUSOGEZEWA JAPO CHUO KIKUU


Dah... pande za SAUT mambo mswano kila mtu yupo bzy na nondoz pande hizi ukipita mida ya jioni ndiyo mpango mzima jamani


Dah... hizi ndizo pande za chuo kikuu cha SAUT kama muonavyo kwenye picha wadau kazi kwenu tukakate nondoz..

MSANII WETU WA KUSINI KATIKA POUZ


Ni msanii kutoka pande za Mtwara anaitwa Dass anakuja kwa kasi sana ktk anga za bongo flavour tuwape sapoti za kutosha jamani wasanii wetu wakusini.

Wednesday, March 24, 2010

DAH...USHER KUGUNDUA KIPAJI CHA JUSTIN BIERBER


Kama hufahamu, Usher ndo kagundua kipaji na kumuingiza kwenye anga za mziki dogo Justin Bierber, na dogo katika fani amekuwa fiti kweli, Usher akaona isiwe tabu, he dicided to surprise him with a brand new Range Rover on his 16th Birthday…jamanii, Justin ameshukuru for the new ride, at sixteen, he will be bowlingggg,dogo saivi marekani anatamba na album yake ya My world Part II, we unakumbuka ulipotimiza miaka 16 zawadi yako ya gharama ilikuwa nini???